Tuesday, December 19, 2017

Jinsi ya Kupata sarafu ya BITCOIN, ETHEREUM, LITECOIN na USD TETHER


Ili kuweza kumiliki na kutumia sarafu za kidigitali utatakiwa uweze kujisajili katika makampuni yanayofanya mabadiliko (exchange) za kifedha za kidigital yaani kwa kimombo huwa zinaitwa forex exchange.

Kuna kampuni ambazo zina toa hiyo huduma unachotakiwa ni kujisajili kisha utaweza nunua na kuuza hizo fedha za kidigitali kwa urahisi zaidi na pia huwa zinatoa wasaa wa kuweza kuhifadhi fedha hizo katika waleti zake (e-wallet) cha muhimu unatakiwa uwe una line ya simu ambayo itatoa huduma za kifedha wakati wa kununua hizi fedha. Hii inamaana kuwa utakapo hitaji kununua hizi fedha utalazimika ulipie kwa kutumia simu yako Mpesa, Tigo Pesa au Airtel Money. Kwa sasa kuna mawakala wanao toa hizi huduma za kuuza sarafu za kidigitali.

Kuweza kujisajili na kununua hizi sarafu  unaweza kuzipata katika website hizi hapa remitano, bitpesa na localbitcoins bonyeza matangazo ili kwenda moja kwa moja katika website husika na kuweza kujiwekea hazina ya dunia ya baadae katika matumizi ya fedha za kidigitali.

No comments:

Post a Comment